29 Julai 2021 - 10:47
Wamarekani wanaanza vita vya kinafsi dhidi ya rais mteule wa Iran

Kundi moja la maseneta wa chama cha Republican nchini Marekani limemtumia barua Rais Joe Biden likimtaka azuie rais mteule wa Iran, Ayatullah Sayyid Ebrahim Raeisi na maafisa wengine wa Iran kuingia nchini humo kwa ajili ya kushiriki mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ikiwa imebakia karibu wiki moja tu kabla ya Sayyid Raeisi kushika hatamu za uongozi, maseneta 6 wa chama cha Republican jana Jumatano walimtumia barua Rais Joe Biden wa Marekani wakimtaka azuie rais mteule wa Iran kushiriki katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliopangwa kufanyika mwezi Sepemba mjini New York. 

Katika barua hiyo maseneta hao wamekariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu wakimtuhumu rais mteule wa Iran kuwa amekiuka haki za binadamu na kutoa wito awekewe vikwazo.

Seneta Tom Cotton wa jimbo la Arkansas ambaye ndiye kiongozi wa kundi hilo amekuwa akiwasilisha miswada ya mara kwa mara akitaka kuzidishwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Mwezi Aprili mwaka huu seneta huyo, akishirikiana na wenzake 14, waliyaandikia barua makampuni matatu na makundi makubwa ya kifedha wakiyatahadharisha juu ya kufanya ushirikiano wowote wa kibiashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iwapo vikwazo vya Marekani vitaondolewa.  

342/